Header Ads

CHELSEA MBIONI KUWEKA REKODI YA DUNIA KATIKA USAJILI

MUDA wowote kuanzia leo klabu ya Chelsea inaweza kuweka rekodi ya dunia katika duru za usajili zinazoelekea ukingoni huko barani Ulaya hii ni baada ya kuripotiwa kuandaa kitita cha £60m kwa ajili ya kutaka kumsajili beki mahiri wa Napoli,Khalidou Koulibaly,25.

Kwa majubu wa habari zilizochapishwa kwenye gazeti la Telegraph la Uingereza ni kwamba Chelsea imefikia uwamuzi huo baada ya kushuhudia ofa zake mbili za awali za £30m na £48 zikikataliwa kwa madai kuwa ni ndogo huku Kocha wake Antonio Conte akisisitiza kuwa anahitaji huduma ya beki huyo katika ujenzi mpya wa kikosi chake.

Ikiwa habari hizo zitakuwa na ukweli ndani yake basi Chelsea itakuwa imeweka rekodi ya kuwa klabu iliyowahi kutumia pesa nyingi zaidi kusajili mchezaji wa safu ya ulinzi duniani na kulizidi dau la £47m lililotolewa na Manchester City wiki iliyopita kumsajili beki John Stones kutoka Everton.

Pia usajili huo utamfanya Koulibaly kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya klabu ya Chelsea na mchezaji ghali zaidi Afrika.Usajili ghali zaidi kwa sasa Chelsea ni ule wa Fernando Torres wa £50m kutoka Liverpool miaka minne iliyopita.

No comments