Header Ads

YANGA SC KUSAKA REKODI HII LEO DHIDI YA TP MAZEMBE

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amesema pamoja na kwamba wameshatolewa kwenye kinyang’anyiro cha michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika,lakini wanalenga kuweka rekodi leo timu yake itakapomenyana na TP Mazembe ya Congo DR.

Yanga leo inamaliza ngwe ya mwisho dhidi ya mabingwa hao wa zamani wa Afrika watakapokutana kwenye uwanja wa Stade TP Mazembe mjini Lubumbashi.

Wawakilishi hao wa Tanzania walitupwa rasmi kwenye michuano hiyo baada ya Medeama ya Ghana kuifunga Mazembe
mabao 3-2 na hivyo kufikisha pointi nane ambazo Yanga haiwezi kuzifikia hata ikishinda mechi ya leo. 

TP Mazembe inaongoza
kundi A ikiwa na pointi 10 ikifuatiwa na Medeama yenye pointi nane na Mo Bejaia ikiwa na pointi tano.
Medeama na Bejaia zitacheza mechi kesho.

Yanga yenye pointi nne, katika mchezo wa kwanza dhidi ya timu TP Mazembe kwenye uwanja wa Taifa ilifungwa bao 1-0.Ikishinda leo itafikisha pointi saba.

Hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa,mwaka 1998 ilifika hatua kama hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa lakini haikushinda mchezo hata mmoja wa makundi.

Mwaka huu inaonekana kuna mabadiliko baada ya kushinda angalau mchezo mmoja dhidi ya TP Mazembe na kupoteza miwili dhidi ya Medeama na Mazembe na kupata sare moja dhidi ya Medeama kwenye uwanja wa nyumbani, Taifa.

Timu zilizoko kwenye kundi moja A,Medeama itachuana na Mo Bejaia nchini Algeria kumaliza mchezo wa mwisho,lakini kama Medeama itashinda au kutoka sare itajiongezea pointi lakini kama Mo Bejaia yenye pointi tano itashinda basi zitalingana kwa pointi, hivyo mshindi huenda akaamuliwa kwa idadi ya mabao.

Kocha Pluijm alisema licha ya kutolewa hakuwezi kuwakatisha tamaa na kushindwa kufanya vizuri katika mchezo wa mwisho.

Alisema ushindi ni muhimu sio tu kwa timu kuweka rekodi bali hata kwa wachezaji watakaocheza kwa juhudi ni nafasi yao kujiuza.

“Tunahitaji kushinda mchezo huu na tunauchukulia kwa ukubwa ili tumalize salama na kujiwekea rekodi ya kipekee,”alisema.

No comments