Header Ads

MUOGELEAJI WA MAREKANI ATISHIWA KUULIWA NA WALINZI WA RIO, BRAZIL

Ikiwa imesalia siku moja kabla ya kumalizika kwa michezo ya Olimpiki inayofanyika nchini Brazil, matukio ya kiharifu yameendelea kuripotiwa ambapo kwa sasa imeripotiwa kutokea kwa mwogeleaji wa Marekani.
Mwogeleaji huyo Gunnar Bentz alitoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram na kuelezea kukutwa na mkasa wa kuvamiwa na watu aliowadhania kuwa ni walinzi wa mji wa Rio wakati alipokuwa katika gari katika moja ya kituo cha mafuta kilicho katika mji huo.
Bentz alielezea kuwa wakati akitaka kuondoka alizuiliwa na watu hao ambao walikuwa wakizungumza lugha ya Kireno na Kiingereza kisha kumnyoshea bunduki wakimtaka atoe pesa ndiyo aruhusiwe kuondoka
“Niliwapa nilichokuwa nacho katika mfuko wangu wa kihafadhia pesa, ilikuwa ni Dola 20, na Jimmy akawapa Reals 100 ambayo ni kama Dola 50,” alisema Bentz.

No comments