Klabu ya Coastal Union imefungua kesi ya madai dhidi ya Simba, Yanga
na Kagera Sugar ikitaka klabu hizo kulipa Sh milioni 75 kwa kuwasajili
wachezaji wake kinyume cha sheria.
Coastal inaidai Simba Sh milioni 30 kama fidia kwa kuwasajili
wachezaji wake Ibrahim Twaha, Hamadi Hamis na Abdi Banda wakati klabu
hiyo iliyoshuka daraja msimu uliopita, ikitaka Yanga kuilipa Sh milioni
20 kwa kumsajili Juma Mahadhi sajili zote zikiwa ni za mwaka 2014/2015.
Pia klabu hiyo yenye maskani yake Tanga inaidai fidia ya Sh milioni
20 klabu ya Mbeya City kwa kuwasajili kinyume cha taratibu wachezaji
wake Ayubu Yahaya na Fikiria Bakari huku Kagera Sugar ikidai Sh milioni 5
kwa kumsajili Ibrahim Twaha na kufanya timu hiyo ya Wagosi wa Kaya
kuvuna Sh milioni 75 iwapo klabu hizo zitakutwa na hatia kwa kusajili
kinyume cha sheria.

No comments