Header Ads

PICHA&VIDEO: MSHIRIKI WA MBIO ZA KUTEMBEA AJISAIDIA KATIKATI YA MASHINDANO.

Mfaransa Yohann Diniz, aliyeshiriki kwenye mashindano ya mbio za kutembea za kilometa 50, amesitaajabisha ulimwengu leo baada ya kamera ya video kumpiga picha akiwa anajisadia haja kubwa kwenye kaptura yake wakati wa mashindano huko Rio kwenye Olimpiki.
Awali kabla ya mashindano kuanza, Mfaransa huyo alilamika kusumbuliwa na tumbo, lakini akaendelea kushiriki mashindano ambapo baada ya muda alianguka nchini na mmoja katika ya washiriki wenzie akamsadia kumnyanyua na wakaendelea na mashindano kabla ya tumbo kumzidia na kuamua kujisadia katikati ya mashindano hayo.
Kabla ya hayo, Yohann Diniz alikuwa akiongoza mbio hizo lakini aliishia kupata nafasi ya 11,licha ya maswahiba hayo yaliyomkuta ya kuanguka njiani na kujisaidia katikati ya mashindano.




No comments