Header Ads

AJIB MCHEZAJI BORA WA WIKI LIGI KUU BARA

Ajib ameibuka mchezaji bora wa wiki Ligi Kuu Bara baada ya michezo ya wikendi ilioisha kwa kuwafunika baadhi ya nyota kadhaa waliokuwa na wiki nzuri
Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars na klabu ya Simba, Ibrahim Ajib ameibuka mchezaji bora wa wiki Ligi Kuu Bara baada ya michezo ya wikendi ilioisha kwa kuwafunika baadhi ya nyota kadhaa waliokuwa na wiki nzuri kama Hassana Kabunda wa Mwadui, Isihaka wa African Lyon,Raphael Alpha wa Mbeya City na wengine waliokuwa na wikendi nzuri kwao
Ajibu ameibuka mchezaji bora wa wiki baada kuonesha kiwango kizuri na cha kusisimua dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons na kuisaidia klabu yake ya Simba kuibuka na alama tatu muhimu katika mchezo huo 

Siku hiyo Ajibu alifanikiwa kufunga goli moja kipindi cha kwanza akipokea pasi aliyo pewa na mshambuliaji Mavugo kabla na yeye ajatengeneza goli la tatu kwa ufundi mkubwa lililofungwa na Mrundi Laudit Mavugo kwa kichwa katika ushindi wa goli tatu kwa bila dhidi ya Tanzania Prisons
Mshambuliaji huyu alikuwa mwiba wa kuotea mbali kwenye safu ya ulinzi ya maafande wa Prisons kwa kuisumbua kila muda na kuipa wakati mgumu kwenye kumzuia, alitengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa wenzake ambazo hawa kuzitumia vizuri

Kwa ushindi huo Mnyama Simba alioupata wikendi hii wamefanikiwa kukwea hadi kileleni mwa msimamo kwa kufikisha alama 51 katika mchezo 22 huku wakimuacha mpinzani wao Yanga kwa alama 2 wenye pointi 49 katika muchezo 21, mchezo moja mkononi

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kilicho anza siku ya Jumamosi dhidi ya Prisons chini ya mwalimu Mcameroon Joseph Omog ni Daniel Agyei, Javier Bukungu, Mohamed Hussein, Method Mwanjale, Lufunga, Muzamiru Yasin, James Kotei, Said Ndemla, Laudit Mavugo, Juma Luizio na Ibrahim Ajib

No comments