Header Ads

BENCHI LA THAMANI ZAIDI DUNIANI

Manchester United ni timu kubwa sana,unapoambiwa kuhusu ukubwa wa timy kuna mambo mengi sana yakujumuishwa hadi timu iwe kubwa.Historia ya timu na idadi ya mashabiki ni kati ya vitu ambavyo vinaifanya timy iweze kuitwa timu kubwa,na kutokana na historia na hali ilivyo sasa Manchester United huwezi iacha ukitaja timu kubwa 4 duniani.
Sasa United wanazidi kuonesha umwamba wao uwanjani na nje ya uwanja.Japokuwa mechi dhidi ya Blackburn Rovers iliwasimamishia rekodi yao ya kucheza michezo mitano mfululizo bila wavu wao kuguswa,lakini mchezo huo unaendeleza rekodi ya Man United kucheza michezo 17 bila kufungwa,idadi hiyo ni kubwa zaidi kwa sasa katika ligi tano Ulaya na anaefuatia ni Barcelona waliocheza michezo 16 mfululizo bila kupoteza.
Achana na hilo sasa kuna hii rekodi mpya United waliyoweka katika mechi dhidi ya Blackburn.Wakati mpira unaanza tulimuona mchezaji ghali kwa sasa Paul Pogba akiwa jukwaani,lakini jukwaa hilo hilo kulikuwa na Luke Shaw ambae nae akiwa na miaka 18 tu alinunuliwa kwa pesa nyingi,Eric Bailly,Juan Mata bila kumsahau King Kadabra wote walikuwa benchi.
Hili ndilo benchi ghali zaidi kuwahi kutokea katika michuano ya FA.Toka kuanzishwa kwa michuano hii hakujawahi kuonekana kukiwa na benchi la gharama kubwa kama hili,benchi hili limeigharimu Manchestet United kiasi cha £192m.Majirani zao Man City walishawahi kuweka rekodi katika mchezo wao mwezi uliopita dhidi ya Crystal Palace baada ya kuwa na benchi lenye thamani ya £162m,ikiwa ni £30m pungufu kwa United.
Paul Pogba alikuwepo jukwaani akiwa na jumla ya thamani ya £89m,Juan Mata alikuwa pembeni yake akiwa na thamani ya
£37m,Luke Shaw £30m,mkongwe Bastian Schwrinsteiger nae alinunuluwa £6m alikuwepi,huku mlinzi Eric Bailly nae akiwa na thamani ya £30m sahau kuhusu Ibrahimovich na golikipa Dean Henderson ambao walikuja kama wachezaji huru.United waliifunga Blackburn na sasa wataenda kukutana na Chelsea katika hatua ya robo fainali.

No comments