Header Ads

BOSSOU MGUU NDANI MGUU NJE YANGA

Inasemekana kuwa hali si shwari  ndani ya klabu ya Yanga kufatia beki wa kimataifa wa Togo Vicent Bossou ambae hakucheza katika mechi ya Jumamosi kutoka na kukorofishana kamati ya hamasa Kwa kuwakumbushia ahadi yake ya malipo  ambayo walimuahidi.
Taarifa za kuaminika kutoka kwa chanzo ndani ya Yanga zinasema: “Bossue aliwaomba viongozi wake wamutatulie matatizo yake mapema kabla ya mechi dhidi ya Simba lakini  hawakufikia mwafaka mpaka  akaondolewa kwenye mipango ya mwalimu dakika za mwisho katika pambano, kwa kuomba alipwe pesa zake.”
Kiongozi mmoja mwenye ushawihi mkubwa ndani ya klabu hiyo alizungumza na shafiidauda.co.tz alisema: “Kwanza tumemvumilia sana Bossou amekuwa anajenga makundi ndani ya wachezaji aliendaga Ulaya kuongea na timu akasema anunue mkataba wake yakamshinda tukampokea kwa mikono miwili na alishavunja masharti ya mkataba ila tukamsamehe ila yeye haoni tumefungwa na Simba ikiwa pungufu wachezaji hawana morali tuna mechi dhidi ya Ruvu kesho kutwa unategemea nini? Liwalo na liwe tu.”
“Kumekuwa na mkanganyiko juu ya wachezaji wa kulipwa na uongozi baada ya Ngoma kulumbana na uongozi kuhusu kuumwa kwake huku  daktari wa timu anasema amepona limebaki jukumu la kocha kumtumia, lakini yeye  Ngoma akaja na daktari wake akasema bado hajapona mkanganyiko ukaibuka.”
Siku za Bossou zinahesabika ndani ya Yanga, leo kutakuwa na kikao ila kitakuwa cha  siri sana kikao hicho ni cha kuweka mambo sawa kuelekea mechi yetu dhidi Ruvu Shooting na mechi ya kimataifa dhidi ya Zanaco March 11, na suala la Bossou litajadiliwa pamoja na mechi ya Simba.”
“Tuna asilimia kubwa ya kuachana na Bossou hata kabla ya kumalizika kwa mkataba wake mwishoni mwa msimu.”

No comments