INIESTA ASEMA WANA IMANI NA ENRIQUE
Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Andres Iniesta amekanusha taarifa kuwa klabu hiyo imepoteza imani juu ya kocha wao Luis Enrique kufuatia matokeo ya kutoridhisha katika siku za karibuni.
Macho yote yalikuwa Nou Camp kuangalia matokeo ya Barcelona dhidi ya Alaves ambapo wakatalunya hao walipata ushindi katika kiwango kisichoridhisha kwa mashabiki na bodi ya klabu hiyo.
“Hatujapoteza imani na kocha wetu, ni moja ya mapito nina uhakika tutarejea katika hali ya ushindi kinachotakiwa ni kujiamini kuwa tutarejea kufanya kitu sahihi,” alisema Iniesta.
GUARDIOLA AKASIRISHWA NA WANAOMPONDA WENGER
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amekasirishwa na kitendo cha mashabiki kumponda kocha wa Arsenal Arsene Wenger na kutaka atimke klabuni hapo akisema kuwa kitendo hicho hakikubaliki.
“Ninachosikia ndani ya siku 10 kutoka kwa wachezaji wa zamani, waandishi wa habari sio sahihi, kazi zetu haziheshimiki ndio maana tunafanya maamuzi tunayotaka,” Guardiola alisema.
Wenger amekuwa katika tetesi za kutimka klabuni hapo kufuatia kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya Bayern Munich katika klabu bingwa barani Ulaya mchezo uliofanyika wiki iliyopita.
DZEKO ASIFIWA NA KOCHA WAKE
Kutokana na kiwango cha hali ya juu cha mshambuliaji Edin Dzeko, kocha wake Luciano Spaletti amemsifia raia huyo wa Bosnia kuwa amekuwa mkali kutokana na kujiamini kwake.
Baada ya kufunga ‘hat trick’ katika mashindano ya Europa ligi aliendeleza makali yake dhidi ya Torino kwa kufunga goli moja katika ushindi wa mabao 4-1 na kufikisha mabao 18 ya ligi kuu nchini Italia.
“Dzeko anajiamini kuwa ni mshambuliaji wa kiwango cha juu na ni faida kwa klabu yetu. Edin alipata wakati mgumu msimu uliopita ila sasa wenzake wamekuwa na imani nae na anafanya vizuri” alisema Spalletti.
BERBATOV ATAKA TIMU IKATAKAYOMPA NAFASI
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Dimitar Berbatov 36, amekiri kutafuta klabu ya kuchezea ili aendelee kucheza soka baada ya kuwa mchezaji huru tangu mwaka 2016.
“Najaribu kutafuta timu ya kuchezea kwa sasa bado najiskia vizuri maana nafanya mazoezi, niliongea na mchezaji mwenzangu wa zamani Jermaine Jenas na alisema ni kiasi gani vigumu kuacha soka” Berbatov aliiambia BBC 5 live sport.
Mshambuliaji huyo alishinda mataji akiwa United huku akiwa mfungaji bora ligi kuu nchini Uingereza akifungana magoli na Tevez.
GABIDOL AFUNGUA AKAUNTI YA MAGOLI MILAN
Mshambuliaji wa Inter Milan Gabidol amejibiwa maombi yake kwa kufunga bao lake la kwanza kwa katika ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Bologna.
“Nina furaha sana kufunga bao langu la kwanza na pia limetupatia ushindi nilikua nikisubiri wakati huu nikijituma na muda umefika nimefunga sitosahau tukio hili” alisema Gabidol baada ya mchezo huo kumalizika.
Gabidol amekuwa katika wakati mgumu klabuni hapo tangu ajiunge akitokea Santos kutokana na kutofumania nyavu kama alivyokua akifanya katika klabu hiyo ya Brazil.
No comments