Harry Kane amefunga magoli matatu yaani hat-trick wakati Tottenham ikitinga robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Fulham.
Kane aliteleza na kuutumbukiza mpira wavuni baada mpira uliorushwa haraka na Kieran Trippier kuipita beki ya Fulham na Christian Eriksen kuupiga krosi mpira huo
Dakika tano baadaye, wachezaji hao watatu wa Tottenham walisaidiana vyema ambapo pasi ya Trippier ilipigwa krosi na Eriksen na Kane kufunga goli la pili.
Kane tena alikamilsha hat-trick yake ikiwa ni ya pili kwa msimu huu na ya tano akiwa na Tottenham akiunganisha pande kutoka kwa Dele Alli.
Harry Kane akiteleza na kufunga goli la kwanza
Harry Kane akiwa ameupiga mpira uliojaa wavuni na kuandika goli la pili
No comments