Kuna baadhi ya nyota walionekana mzigo kwenye duru la kwanza Ligi Kuu Bara, walishindwa kabisa kulishawishi benchi la ufundi na kupelekea kusugua benchi kwa mzunguko mzima na wengine kugikiriwa kuachwa mwishoni mwa msimu
Ila mambo yamekuwa tofauti mzunguko wa pili, wale walioonekana mzigo mwanzo ndiyo wamekuwa ni msaada katika timu raundi hii ya pili
Zote kali sports inakuletea baadhi ya nyota ambao wameibukia kuwa msaada mzunguko wa pili baada ya kusugua benchi duru la kwanza kwenye Ligi Kuu
Obrey Chirwa - Yanga
Usajili wake ulitikisa hapa nchini kutokana na dau kubwa lililo mvuta Jangwani kutoka Fc Platnums ya Zimbabwe, maisha ya mshambuliaji huyu mwanzoni hayakuwa mazuri kwake, ilishindwa kabisa kuendana na kasi ya klabu na kuishia kusugua benchi mzunguko wa kwanza karibu wote na kidogo atemwe dirisha dogo, ila tangu raundi ya pili imeanza amekuwa ni mtu tofauti kabisa hivi karibuni amekuwa msaada ndani ya kikosi kwa kufunga magoli muhimu
Laudit Mavugo - Simba
Alianza vizuri Ligi kabla ajapoteza nafasi kikosi cha kwanza na kupelekea kusugua benchi, Mrundi huyu ilifikia kipindi akawa ana zomewa na mashabiki wake pindi akigusa mpira, ila taratibu mambo yameanza kumnyookea sasa, anafunga magoli na pia ana toa pasi za magoli kwa wenzake, tayari ameanza kurudisha imani kwa mashabiki wa klabu yake
Said Ndemla - Simba
Takribani mwaka nzima kiungo huyu mshambuliaji amekuwa na wakati mgumu kuanza ndani ya kikosi cha kwanza cha Wekundu wa Msimbazi, nafasi yake ya kucheza ilikuwa mpaka pindi mchezaji aumie au aingie kutokea benchi, tangu mzunguko wa pili uanze mwalimu Omog amekuwa akimtumia Ndemla kwenye eneo la kiungo na mchezaji huyu aja muangusha hata kidogo kwenye mechi hizo, amekuwa bora sana hasa kwenye kuiunganisha idara ya ulinzi hadi ushambuliaji
Juma Kaseja - Kagera Sugar
Hakufanikiwa kucheza hata mchezo mmoja mzunguko wa kwanza akiwa Mbeya City na kupelekea kuachwa, duru la pili mlinda mlango huyu ameamua kujiunga na Kagera kwa ajili ya raundi hii ya mwisho, tangu aanze kuitumikia Kagera mzunguko wa pili ameonesha ubora wa hali ya juu na kuwashangaza wengi waliokuwa wakiamini uwezo wa nyanda huyo umeisha

No comments