Klabu ya Hull City inashiriki Ligi Kuu ya Uingereza maarufu EPL, imeichapa timu iliyosheheni wachezaji kutoka vilabu mbalimbali chini Kenya (Kenya All Stars) kwa mabao 2-1.
Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa jumatatu usiku kwenye uwanja wa KCom jijini Hull, na wenyeji kutangulia mbele kwa mabao mawili haliyofungwa na Elliot Holmes kabla ya beki wa Kenya Haroun Shakava kujifunga bao la pili.
Kenya All Stars ilifanya mashambulizi kazaa kupitia kwa washambuliaji wake, Moses Odhiambo, Makwata na Allan Wanga bila mafaniko, mpaka kiungo Humphrey Mieno alipoitia timu yake bao la kufutia machozi kwa mkwaju mkali nje ya eneo la hatari.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya matunda ya wadhamini wa Hull City kampuni ya michezo ya kubahatisha SportPesa yeye makao makuu yake nchini Kenya, Mwezi July Hull City watakua nchini Nairobi kwa kucheza mchezo wa marudiano na kikosi hicho cha Kenya All Stars.
No comments