Nyota wa muziki wa Adele anaonekana kukataa tuzo ya Grammy aliyotunukiwa kwa kuwa na albamu bora zaidi.
Badala yake, amesema Beyonce ndiye aliyestahiki zaidi kutunukiwa tuzo hiyo.
Adele alipewa tuzo hiyo kwa albamu yake kwa jina 25 ambayo imevuma sana
duniani, lakini ameambia waliohudhuria kwamba, "Haiwezekani kwangu
kupokea tuzo hii".
"Ni heshima kubwa sana kwangu na nashukuru, lakini Beyonce ndiye mwanamuziki bora maishani mwangu".
Ushindi wa Adele dhidi ya Beyonce bila shaka utachocheza zaidi malalamiko kwamba tuzo za Grammy sana huwabagua wasanii weusi.
Wasanii kadha wakiwemo Frank Ocean na Kanye West, waliamua kususia
sherehe za mwaka huu za kutoa tuzo kwa washindi kwa msingi huo.
Ocean hata alikataa kuwasilisha albamu yake maarufu ya Blonde ishindanie
tuzo akisema tuzo za Grammy hazionekani "kuwakilisha vyema watu wa eneo
ambalo nimetoka mimi, na kudunisha watu ambao ninadunisha".
Miaka miwili iliyopita, West aliondoka kwa hasira jukwaani baada ya
Beyonce kukosa kutangazwa mshindi kwa albamu yake kwa jina Beck's
Morning Phase.
Hata hivyo, albamu ya Adele ya 25 bila shaka ndiyo iliyouza nakala
nyingi zaidi miongoni mwa zilizokuwa zinashindania tuzo hiyo. Iliishinda
albamu ya Lemonade yake Beyonce kwa 10 kwa 1.
Haijabainika iwapo Adele ataikataa rasmi tuzo hiyo.
Iwapo atafanya hivyo, basi itakuwa ni mara ya pili pekee kwa jambo kama hilo kutokea.

No comments