Header Ads

KOCHA WA SOUTHAMPTOM AOMBA TEKNOLOJIA YA OFFSIDE

Baada ya kupoteza dhidi ya klabu ya Manchester United kwenye mchezo wa Fainali ya EFL, kocha wa klabu ya Southampton amedai kuwa klabu yake ilinyongwa na walistahili kutendewa haki kutokana na kukataliwa kwa goli la Manolo Gabbiadini ambalo lingewafanya kuongoza kabla ya ZLatan kufunga mpira adhabu.
Kocha huyo ameomba kuwepo kwa teknolojia ya kugundua offside kama ilivyokuwa goal line technology. Claude Puel amesema kumbukumbu huwa ni za walioshinda na mambo mengine usahaulika lakini ana furaha wachezaji wake walicheza vyema.
Gabbiadini alifunga mara mbili kwenye mchezo huo na Puel anaamini kuwa wangeumaliza mchezo kama goli lile lingekubaliwa kwani pia walicheza vyema zaidi kuliko wapinzani wao hao ambao walitwaa ubingwa kutokana na ubora wa Zlatan Ibrahimovic aliyefunga mabao 26 sasa kwenye mashindano yote.
“ningependa kuwepo kwa teknolojia ya offside siku zijazo ili kuondoa tatizo hili lililotukuta. Kuna nyakati maamuzi mabovu yanakuwa dhidi yetu hivyo ianatubidi kukubaliana na khali tu kwa sasa.”
Zlatan Ibrahimovic alikuwa anatwaa taji lake la 32 kwenye historia ya maisha yake ya Soka. Ikumbukwe kuwa goalline technology ilianza kutumika kwenye ligi kuu ya Uingereza mwanzo wa msimu wa 2013-2014.

No comments