Kiungo wa kimataifa wa timu ya Taifa Uganda ‘The Cranes’ Khalid Aucho amejiunga na washindi wa Ligi ya Mabingwa 1990/1991 klabu ya Red Star Belgrade ya nchini Serbia.
Aucho ambaye alikua kwenye michuano ya Mataifa Afrika (AFCON) Gabon na kikosi cha Uganda, alitemwa mapema Januari 2017 na klabu yake ya Baroka FC inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini pamoja na Geofrey Massa.
Kabla ya kujiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini Agosti mwaka jana, Aucho aliibukia Jinja Manispaa kabla ya kujiunga na Simba ya Uganda na baadae kwenda Kenya kuzicheza klabu za Tusker na Gor Mahia FC.
Red Star Belgrade ndio pekee yenye mafanikio kutoka Ulaya Magharibi kwa kufanikiwa kutwaa Ligi ya Mabingwa, ikicheza fainali ya Kombe la Mabingwa 1978 na mchezo wa UEFA Super Cup 1991.
Kufuatia Aucho kujiunga na klabu hiyo, kunafanya idadi ya wachezaji wa Uganda wanaocheza nje ya nchi kuongezeka, kwani mpaka sasa ina wachezaji zaidi ya 30 wanaocheza nje ya Uganda.
No comments