Manchester City wana kila sababu ya kuwa na wasiwasi na wapinzani wao wa raundi ya 16 bora ya Champions League – Monaco, timu ambayo imepoteza hatua moja tu ya mtoano ya ulaya vs Timu za EPL.
• Monaco wamefikia hatua ya mtoano baada ya kuongoza Kundi E, wakati City walifuzu wakiwa washindi wa pili wa Kundi C nyuma ya FC Barcelona.

• City wanatafuta nafasi ya kufuzu kucheza robo fainali kwa mara ya pili katika historia yao, kufuatia kufuzi msimu uliopita na kuvuka mpaka nusu fainali.
• Hawajapoteza mchezo hata mmoja kati ya 9 iliyopita ya UEFA Champions League iliyochezwa katika uwanja wao wa nyumbani – (W6 D3).
• City waliwaondoa Paris Saint-Germain katika robo fainali msimu uliopita, Kevin De Bruyne akifunga magoli katika sare ya 2-2 Parc De Princes na goli la ushindi katika mchezo wa pili wa 1-0 jijini Manchester.
• Josep Guardiola ameshinda mechi zote 7 zilizopita za raundi ya 16 bora akiwa kocha wa Barcelona na FC Bayern Munchen.
Monaco

• Monaco wanatafuta nafasi ya pili ya kufuzu robo fainali ya UEFA Champions League ndani ya misimu mitatu, walicheza robo fainali mwaka 2015 baada ya kuwafunga Arsenal FC kwa matokeo ya 3-1 na 0-2.
• Wameshashinda kwenye ardhi ya Uingereza mara 1 katika msimu huu, waliwafunga Tottenham Hotspur 2-1 katika uwanja wa Wembley katika mchezo wa ufunguzi, magoli ya Bernado Silva na Thomas Lemar yakiwapa ushindi wa 2-1 tena nyumbani.
• Rekodi ya Monaco ugenini dhidi ya vilabu vya Uingereza inaonyesha W4 D2 L2.
• ASM wameshinda mechi zote kasoro moja kati ya tano za mechi za mtoano dhidi ya vilabu vya Uingereza, ukiwemo mchezo wa robo ya Champions League dhidi ya Manchester United msimu wa 1997/98, Chelsea FC (2003/04 semi-final) na Arsenal FC (2014/15 round of 16.)
No comments