Header Ads

MPIRA UTAKAOTUMIKA KWENYE HATUA ZINAZOFUATA UEFA WATANGAZWA

Kuelekea kuanza kwa mechi za hatua ya mtoano, 16 bora ya klabu bingwa barani Ulaya, kampuni ya Adidas leo Jumatatu imetangaza toleo la mipira mipya itakayotmika kwenye hatua zilizobaki za mashindano.
Ikiwa mechi ya Fainali itafanyika nchini Wales, ambao wataandaa mchezo huu katika uwanja wa Princpality, mpira huo utakuja na aina mpya muonekano wa kuvutia ikiwa na mapambo ya mnyama anayefahamika kama dragon.
Matengenezo ya mpira huo yamezingatia muonekano wa bendera ya Taifa hilo, ambayo katika bendera hiyo kwenye bendera hiyo kuna picha ya mnyama huyo ikinakshi bendera.
Timu ya adidas, ambayo ilisafiri mpaka Cardiff ikiwa ni sehemu ya kuweka sawa matengenezo ya mipira hiyo imesukumwa kutumia muonekano huo kutokana na nguvu na uwezo ambayo mnyama Dragon uwakilisha katika maisha ya kila siku na imani zilizokuwepo.
Mpira umetengenezwa katika namna ambayo itaruhusu kila mchezaji kuutumia kutokana na aina yake ya uchezaji hasa mastaa wengi wakiwemo Lionel Messi, Luis Suarez, Cristiano Ronaldo na aina ya akina Thomas Muller.
Barcelona's deadly trio will get a feel for the ball when they play Borussia Dortmund
Mpira huo ambao umelenga maadhi ya nchi ya Wales, utatumika kwa mara ya kwanza siku ya Jumanne ambapo mechi za hatua ya 16 bora zitaanza kwa mara ya kwanza.
Benfica vs Borussia Dortmund na Paris Saint-Germain dhidi ya Barcelona zitakuwa mechi za kufungua hatua hii.
Real Madrid will be looking to retain their Champions League crown at the Principality Stadium
Na utamu wa michezo hii hautoishia hapo kwani Bayern Munich watakuwa wenyeji wa Arsenal siku ya Jumatano huku Real Madrid wakicheza na Napoli kwenye uwanja wa Bernabeu.
Na mpira huo wa adidas utatumika katika kila mchezo ikiwemo fainali itakayochezwa mwezi June tarehe 3 huko Cardiff.

No comments