Amesema anatambua kuwa michuao hiyo nimigumu sana lakini kama mshambuliaji aliyebeba imani za mashabiki wa timu hiyo amejipanga kufunga mabao mengi
Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma amewapongeza wachezaji wenzake ushindi mnono, walioupata katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Ngaya Club ya Comoro.
Ngoma ameiambia Goal, ushindi huo ni mwanzo mzuri kwao katika mikakati yao ya kucheza fainali za michuano hiyo kwa mwaka huu baada ya mwaka jana kuishia hatua ya makundi.
“Nafurahi kuona tumeanza vizuri na kuonyesha dhamira yetu ya kucheza fainali za ligi ya mabingwa mwaka huu, hakuna linaloshindikana kwasababu Yanga tuna kikosi bora ambacho kinawachezaji wenye uzoefu hivyo naamini kama tukikaza kama tulivyokusudia tunaweza kufanikiwa,”amesema Ngoma.
Mshambuliaji huyo ambaye amegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo, alisema hali yake kwa sasa inaendelea vizuri na kuna uwezekano mchezo wa marudiano atakuwepo uwanjani ili na yeye aweze kutoa mchango kwa timu yake katika michuano hiyo.
Amesema anatambua kuwa michuao hiyo nimigumu sana lakini kama mshambuliaji aliyebeba imani za mashabiki wa timu hiyo amejipanga kufunga mabao mengi zaidi ya ilivyokuwa mwaka awamu iliyopita ambayo alifunga mabao manne .
“Nimejipanga kuhakikisha awamu hii nafunga mabao mengi zaidi ya ilivyokuwa mwaka jana, kwasababu ubora wa timu umeongezeka lakini hata nafasi ambayo kocha amekuwa akinipanga inaniruhusu kufanya hivyo,” amesema Mzimbabwe huyo.
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-1, mchezo ambao Ngoma aliukosa kutokana na kuuguza maumivu ya nyonga aliyoyapata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Stand United Ngoma na kusababisha aondolewe kwenye kikosi kilicho kwenda Comoro.
No comments