Kiungo wa Yanga na nahodha msaidizi wa klabu hiyo Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ amesema safari ndio kwanza imeanza na ushindi wa magoli 5-1 walioupata ugenini haukuja kirahisi bila bali ni kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na wachezaji kwa ushirikiano na benchi la ufundi.
“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababui hakuna mchezo mdogo, tumeshinda kwa magoli 5-1 ni jambo la kumsukuru Mungu na pia niwapongeze wachezaji wenzangu kwa ujumla kwa sababu tumeonesha kwamba ulihitaji ushindi na ukicheza ugenini inakuwa sio rahisi lakini mwisho wa siku tunashukuru tumepata pointi tatu na kuanza mashindano haya vizuri,” – Haruna Niyonzima.
“Nawashukuru pia mashabiki waliokuwepo uwanjani pamoja na wale wa Dar es Salaam ambao hawakuweza kufika naamini walituombea dua. Safari ndio inaanza, tunajipanga vizuri kwa uwezo wa Mungu tukirudi naamini mchezo wa pili utakuwa mzuri.”
“Nawapongeza pia watu wa benchi la ufundi kwa sababu wote tumefanya kazi kwa ujumla na tumeweza kuibuka na ushindi mkubwa ambao haukua ushindi rahisi.”
Matokeo hayo yanaiweka Yanga kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele kabla ya mchezo wa marudiano ambao utapigwa uwanja wa taifa majuma mawili yajayo.
No comments