Timu ya Real Madrid imetokea kufungwa goli moja nyuma na kufanikiwa kuifunga Napoli magoli 3-1 katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16.
Wageni Napoli walipata goli la kuongoza baada ya kipa Keylor Navas kushtukizwa na shuti murwa lililopigwa na Lorenzo Insigne na kuandika goli ndani ya dakika nane.
Real Madrid ilisawazisha kupitia kwa Karim Benzema kwa mpira wa kichwa, huku Toni Kross akiongeza la pili kabla ya Casemiro kufunga goli la tatu.
Mpira uliopigwa kwa kichwa na Karim Benzema ukielekea golini
No comments