
Camera ya shaffihdauda.co.tz haikupitwa na tukio hilo, ikazinasa picha za kile kilichokuwa ninatupwa na Chirwa kutoka kwenye mlingoti wa goli.
Baada ya kufatilia ikabainika kilichokuwa kinafukiwa kwenye mlingoti wa goli ilikuwa sarafu ya senti tano ya kitanzania (ya zamani) ambapo Chirwa aliitoa mara mbili kwenye magoli yote katika vipindi tofauti (kipindi cha kwanza na kipindi cha pili).

Mara baada ya mchezo kumalizika nikamtafuta Said Mmadi golikipa wa N’gaya ambaye mara zote ndiye alikuwa akifukia sarafu hizo golini kwake kabla ya mchezo kuanza.
“Nilikuwa nafanya vile kwa ajili ya kuwapumbaza wachezaji wa Yanga na kuwatoa mchezoni kisaikolojia ili waamini wanashindwa kufunga kwa sababu kuna nguvu flani pale goli,” alisema Mmadi.
“Hakukuwa na jambo jingine la ziada ndio maana utaona mara nyingi wachezaji wa Yanga walikuwa wanakuja golini kupekuwa kutafuta nilichokiweka golini.”

Kuhusu kuruhusu magoli mengi katika mchezo wa kwanza, Mmadi amesema alikuwa akiwasikia Yanga kuwa walifuzu kucheza hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika hivyo alikuwa na presha kubwa na hofu wakati wa mchezo wa kwanza.
No comments