Issue inayo-trend kwa sasa kwenye soka la Bongo ni game ya February 25, 2017 Simba vs Yanga mchezo uliobeba historia ya soka la Tanzania.
Kuelekea pambano hilo, nakutelea baadhi ya takwimu zinazo husiana na timu hizi mbili lakini takwimu hizi zimejikita zaidi kwenye ligi ya msimu huu (2016/17).
Simba
Inaongoza ligi ikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 22, imeshinda mechi 16, imetoka sare mara tatu na kupoteza mechi tatu.
Kikosi cha Simba chini ya Joseph Omog kimefanikiwa kufunga magoli 36 huku safu yao ya ulinzi ikiruhusu nyavu zao kutikiswa mara saba magoli machache zaidi ya timu yoyote kwenye ligi msimu huu.
Katika mechi tatu ligi zilizopita, Simba imeshinda mechi mbili na kupoteza mechi moja (Simba 0-1 Azam, Majimaji 0-3 Simba na Simba 3-0 Tanzania Prisons).
Lakini Simba imeshinda pia mchezo wake wa FA Cup (Simba 1-0 African Lyon) na kuifanya kuwa imeshinda mechi tatu mfululizo katika mashindano yote.
Yanga
Mabingwa watetezi wa taji la VPL wao wanakamatia nafasi ya pili mwenye msimamo ligi wakiwa na pointi 49 pointi mbili nyuma ya mnyama, Yanga wana mchezo mmoja wa kiporo uliotokana na wao kucheza mechi za kimataifa.
Yanga imepata pointi 49 baada ya kucheza mechi 21 ikizidiwa mchezo mmoja na Simba.
Vijana wa George Lwandamina wametupia nyavuni jumla ya magoli 46 (timu iliyofunga magoli mengi zaidi kwenye ligi msimu huu) huku wao wakiwa wamefungwa magoli tisa katika mechi 21 walizocheza.
Yanga imeshinda mechi 15, imetoka sare mara nne na kupoteza michezo miwili (Stand United 1-0 Yanga na Mbeya City 2-1 Yanga).
Katika mechi tatu za mwisho za ligi, Yanga imeshinda mechi zote (Majimaji 0-1 Yanga, Yanga 2-0 Mwadui na Yanga 4-0 Stand United).
Kumbuka pia Yanga imecheza mechi mbili mfululizo za kimataifa (klabu bingwa Afrika) na kufunga jumla ya magoli 6 huku yenyewe ikiruhusu magoli mawili katika mechi hizo mbili.
Yanga iliifunga N’gaya 5-1 ugenini lakini nyumbani ikatoka sare ya kufungana 1-1.
Head to head (mechi zaba (7) za mwisho) zilizokutanisha Simba vs Yanga
20/10/13 Simba 3-3 Yanga
19/04/14 Yanga 1-1 Simba
18/10/14 Yanga 0-0 Simba
08/03/15 Simba 1-0 Yanga
26/09/15 Simba 0-2 Yanga
20/02/16 Yanga 2-0 Simba
01/10/16 Yanga 1-1 Simba
25/02/2017 Simba ?? Yanga
Wafungaji wenye magoli mengi Simba vs Yanga
Yanga
Simon Msuva (mzawa) ndiye anaeongoza kwa kupachika mabao, tayari ameshachezezesha nyavu mara 10 kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara.
Simba
Mrundi Laudit Mavugo ndiye anaongoza kwa kuwa na magoli mengi kwa upande wa Simba, amefunga magoli 6 (magoli manne pungufu kwa Msuva).

No comments