Header Ads

TETESI KUBWA ZA USAJILI DUNIANI

MPIRA WA FAINALI KLABU BINGWA WAANZA KUTUMIKA
Baada ya kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo Adidas kuzindua rasmi mpira utakaotumiwa katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya hatimaye mpira huo umeanza kutumika.
Mpira huo ukiwa na alama ya mnyama ‘dragon’ kama ishara ya bendera ya nchi ya Wales utatumika katika fainali hizo Juni 3 katika dimba la manispaa ya Cardiff.
Mpira huo umeanza kutumika katika mechi za hatua ya 16 bora zilizowakutanisha PSG dhidi ya Barcelona nchini Ufaransa ambapo wenyeji walishinda mabao 4-0 pia katika dimba la Doa Sport Lisboa Wenyeji Benfica wakipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Borrusia Dortmund.
WAKALA WA VERRATTI AWAONYA PSG
Wakala wa kiungo wa PSG Marco Verratti, Donato Di Campri ameionya klabu hiyo kuwa nyota huyo atatimka Ufaransa endapo klabu hiyo itashindwa kutwaa taji la klabu bingwa barani Ulaya.
“Siyo suala la kumuuza Marco kwa bei yoyote bali yeye anataka kushinda taji hili na kama hii haiwezekani akiwa PSG basi yeye atafanya hivyo mahali pengine” alisema Di Campri.
Verrati amekuwa akihusishwa na klabu za Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich huku akisema anatamani kuichezea Barcelona katika siku za usoni.
KESSIE AFURAHIA KUHUSISHWA NA MAN UTD, CHELSEA
Kiungo wa Atlanta raia wa Ivory Coast Franck Kessie amefurahishwa na tetesi za kuhusishwa na kutaka kujiunga na timu za Manchester United na Chelsea ila ana furaha klabuni hapo.
“Nasoma kwenye vyombo vya habari na nafurahishwa klabu za kiwango cha juu kunihitaji, hii inaonyesha kuwa nina msimu mzuri na nitazidi kufanya vizuri ila nisingependa kuondoka haraka hivi” alisema Kessie.
Kiungo huyo amezivutia klabu nyingi barani Ulaya zikiwemo United, Chelsea, Arsenal, AS Roma na PSG zote zimeonesha nia ya kumsajili kiungo huyo mwenye miaka 20.
DYBALA KUSAINI MKATABA MPYA
Mkurugenzi wa klabu ya Juventus Giuseppe Marotta amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani nyota wao Paul Dybala atasaini mkataba mpya hivi karibuni.
“Wasaidizi wa Dybala wapo Argentina kwa sasa hivyo hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi, mwishoni mwa mwezi watarejea na ndiyo muda wa kusaini mkataba” alisema Marotta.
Nyota huyo raia wa Argentina amekuwa akihusishwa na klabu za Real Madrid na Barcelona ambazo zipo karibu zaidi zikifuatilia suala la mkataba wake na Juventus.
GABIDOL ANA FURAHA MILAN
Kiungo mshambuliaji wa Inter Milan Mbrazil Gabriel Barbosa maarufu kwa jina la ‘GABIDOL’ amesema ana furaha klabuni hapo akikanusha tetesi za kutaka kutimkia Liverpool.
“Ni baridi sana ila nina furaha hapa, wenzangu wananipa mawazo na nafurahi kucheza na nyota ambao nilikua nikiwaona kwenye video. Goli langu la kwanza litakuja tu pale Mungu atakapotaka kwa sasa ni kujituma zaidi na kuisaidia timu,” alisema Gabidol.
Mbrazil huyo ambaye bado hajafunga bao tangu atue Inter akitokea Santos amehusishwa na majogoo wa Anfield Liverpool kutokana na mashabiki wa klabu hiyo kutoridhika na kiwango ambacho walitegemea angekionyesha.
MAN UTD WALIMTENGEA DAU MULLER
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich Jan-Christian Dreesen amekiri kuwa klabu ya Manchester United ilitenga dau la euro 100 milioni kwa ajili ya mshambuliaji wao Thomas Muller.
“kulikua na kitu kama hicho fax ilitokea Uingereza lakini kwetu kumuuza Muller ni jambo ambalo hatujawahi kulijadili.Kama mchezaji anatufaa sisi hatuwezi kumuachia kwa kigezo cha faida wakati tunaweka mapungufu katika klabu,” alisema mwenyekiti huyo.
Muller akiwa katika msimu wake wa tano na Bayern amejikuta akipata wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Carlo Ancelotti na huenda ikawa muda sahihi kwa yeye kufikiria ofa ya United pindi wakimrudia.

No comments