Header Ads

TETESI NA HABARI ZA USAJILI BARANI ULAYA

MASHABIKI CHILE KUANDAMANA SANCHEZ AONDOKE ARSENAL
Maelfu ya mashabiki nchini Chile wameandaa maandamano ya kumshinikiza mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez atimke klabuni hapo.
Mashabiki wanaotazamiwa kufika 4,000 wanategemea kuandamana Machi mosi kufuatia klabu ya Arsenal kudhalilishwa kwa kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Bayern Munich.
Wakitumia ukurasa wa Facebook waliandika “Sisi Wachile tumechoka kushuhudia mmoja wa nyota wetu akijituma peke yake uwanjani kuiwezesha timu hiyo kusonga mbele, hatutaki acheze Real Madrid au arudi Barcelona bali timu nzima ijitume katika kupata matokeo”.
HATUTOMSAJILI VERRATTI ASEMA MAROTTA

Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Juventus Giuseppe Marotta amesisitiza kuwa kiungo wa PSG Marco Verratti hatosajiliwa na klabu yake kama tetesi zinavyovuma.
Verratti ambaye amesaini mkataba mpya na matajiri hao wa Ufaransa mwezi Agosti ameendelea kuhusishwa na klabu ya Juventus kwa muda sasa.Tetetsi zimekuwa zikivuma kuwa huenda akajiunga na mabingwa hao wa Serie A ila mkurugenzi huyo amekanusha taarifa hizo.
Akizungumza na Mediaset Marotta alisema “Namkubali pia ni mmoja wa wachezaji wa timu yetu ya taifa,ni mchezaji mzuri tunayempenda na haitokuwa sawa kumfikiria kwani PSG wanamtegemea na hatuna nafasi”
Verratti alikuwa bora zaidi katika kuiangamiza Barcelona mabao 4-0 mjini Paris katika mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya katikati ya juma.
BARCELONA WAMNASA MINA

Taarifa kutoka gazeti la Mundo Deportivo zinaarifu kuwa klabu ya Barcelona imefikia makubaliano na klabu ya Palmeiras kumsajili beki Yerry Mina.
Wawakilishi wa Barcelona walisema wamekutana na Palmeiras Alhamisi na kufikia makubaliano hayo yatakayomfanya beki huyo kujiunga na mabingwa hao wa La Liga mwaka 2018.
Mina atajiunga na miamba hiyo kwa dili la euro 9 milioni ambapo beki huyo mwenye miaka 22 ameweza kuiwakilisha Colombia katika michezo mitano pia akitajwa kuwa katika timu bora ya ligi ya Brazil.
VASCO DA GAMA YAMNASA FABIANO

Mshambuliaji wa zamani wa Sao Paulo na Sevilla Luis Fabiano amejiunga na Vasco Da Gama akitokea Tianjin Quanjian ya China.
Fabiano 36 alifurahia wakati wake akiwa Sevilla na Sao Paulo amerejea nchini kwao Brazil kwa usajili wa paundi 8 milioni katika klabu ya Vasco Da Gama.
Fabiano akiwa na miaka 19 alianza kukipiga Sao Paulo na kufunga zaidi ya magoli 200 huku akitua Sevilla na kuifungia magoli 72 katika michezo 149 kabla hajajiunga na Tianjin Quanjian ambao aliisaidia kupanda daraja kwa kupachika mabao 23 mbali na hayo alifanya vizuri akiwa na timu ya taifa ya Brazil kwa kufunga mabao 28 katika mechi 45 kuanzia mwaka 2003 hadi 2013.
SOUTHAMPTON YAMNYAKUA CACERES
Klabu ya Southampton imetangaza kumnasa mchezaji wa zamani wa Barcelona na Juventus Martic Caceres kwa uhamisho huru hadi mwishoni wa msimu huu.
Raia huyo wa Uruguay alikua huru tangu aachane na Juventus na kuwa katika mazungumzo na klabu mbalimbali huku akikataa ofa ya AC Milan.
Baada ya kusaini mkataba Caceres alisema “Nina furaha kusaini katika moja ya klabu muhimu katika soka la Uingereza nina hamu ya kujiunga na wenzangu, maamuzi yangu sahihi ni kusaini hapa nina furaha kwa hilo”.

No comments