Header Ads

ULIYAONA HAYA WAKATI MAN U ILIPOCHEZA NA ROVERS

Goli la Zlatan Ibrahimovich limeipeleka United kinywani mwa Chelsea katika mchezo wa robo fainali.United wamefanikiwa kuifunga Blackburn Rovers ikiwa ni mechi 10 mfululizo za FA bila kufungwa.Lakini kuna mambo kadhaa yalionekana katika mchezo huo ila mambo haya makuu manne yalionekana upande wa Manchester United.
LUKE SHAW NA MOURINHO MMMH.
Mwanzoni mwanzoni kulikuwa na tetesi kwamba Mourinho na Luke Shaw wana tofauti,pengine ukumbuke kwamba Shaw alishawahi kutupiwa kijembe mara tuu aliposajikiwa United kipindi hicho Mou yuko Chelsea aliuponda usajili wa Shaw kutoka Southampton kwenda United.Msimu huu ameanza mechi 6 tu za Epl na 3 za Europa na alitarajiwa kuanza dhidi ya Blackburn lakini alikaa benchi,hii inaleta hali ya sintofahamu kuhusu maisha ya baadae ya Shaw ndani ya United.
RASHFORD ANA BAHATI NA MOU.
Kumekuwa na maneno mengi juu ya uwezo wa sasa wa Rashford,amekuwa hayupo kwenye ile fomu aliyokuwa nayo chini ya Van Gaal.Anaonekana kiwango kimeshuka,na wengi wanaona anastahili kukaa benchi huku Mfaransa Anthony Martial akichukua nafasi yake.Lakini Rashford bado anaaminiwa na Mourinho,katika mchezo huu alitolewa dakika ya 88 akiwa ameshafunga golu la kusawazisha.
USAJILI ALIOFANYA MOURINHO NI TIBA UNITED.
Mualmernia Henrikh Mhkitaryan alikuwa mchezaji bora wa mchezo huo,lakini unaweza kuona maingizo mapya klabuni hapo yanavyoibadilisha Manchester United.Sub iliyofanywa kwa kumtoa Martial kumuingiza Zlatan na kumtoa Lingard kumuingiza Pogba ndio ilileta bao la ushindi kwa United.Pasi ya Pogba ilizalisha bao linaloipeleka United Stamfird Bridge kupambana na vinara wa ligi kuu timu ya Chelsea.
MOURINHO HATAKI UTANI KATIKA KILA MECHI.
Siku chache zilizopita Jose Mourinho aliwarushia kijembe makocha wenzake kwa kuwaambia hawako serious na michuano ya FA.Lakini kwa Jose inaonekana amedhamiria haswa kubeba kombe hili.Hakikuanza kikosi cha kwanza lakini katika benchi lao walionekana mastar wengi ambao muda wowote wangeingia ingekuwa balaa.
Na kweli baada ya Blackburn kuongoza na Rashford kuisawazishia United,Mourinho alihitaji kuiua mechi hiyo ndipo alipowanyanyua mastaa wawili Pogba na Ibrahimovich wakaenda wakaua mchezo,benchi la United wachezaji waliokuwepo ilionesha wazi kwamba Mourinho aliwafuata Blackburn kikazi zaidi.

No comments