Header Ads

ZLATAN NA GUNDU LA UEFA

Zlatan Ibrahimovic ni mchezaji mwenye mafanikio makubwa kwenye maisha yake ya soka barani Ulaya lakini kuna kitu ambacho kinaendelea kumtesa hadi leo nacho ni taji la Champions League.
Mshambuliaji huyu mwenye ‘mwili nyumba’ na misuli iliyojengeka vizuri, ameshashinda mataji 10 ya ligi mbalimbali kwenye maisha yake ya soka akiwa na vilabu tofauti maarufu vya Ulaya.
Muda wake wa kucheza soka unazidi kukimbia, lakini wakati yupo PSG kabla ya kujiunga na Manchester United kikosi kikosi hicho kilikuwa na mastaa wenye uwezo wa kushinda taji la Uefa Champions League.
Ibrahimovic amekuwa akipishana na taji hilo, kila anapotoka msimu unaofuata wananyanyua ndoo ya UEFA.
2009 Ibrahimovic aliondoka Inter Milan kwenda Barcelona, 2010 Inter Milan wakashinda UCL, 2010 akaondoka zake Barcelona mwaka uliofata Barcelona wakatwaa ndoo ya UCL. Mwaka 2016 akaachana na PSG na kujiunga na Mashetani wendu Manchester United, je 2017 PSG watachukua UCL?

Chanzo shafy Dauda

No comments