Nyon, Uswisi. Brazil imekuwa timu ya kwanza kufuzu mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 jambo lililoiwezesha kwa mara ya kwanza kupanda kwenye rekodi za dunia za Shrikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) baada ya miaka sita kupita.
Katika msimamo ambao utachapishwa wiki ijayo, miamba hao wa Amerika Kusini wamerudi kwa kasi baada ya kuwa vinara wakiwa ndiyo timu ya kwanza katika kundi lake lenye timu tisa.
Kipindi hicho chote cha mashindano, wamefanikiwa kuziona nyavu mara 25 baada ya kuifunga Paraguary mabao 3-0 Jumanne wiki hii, huku wakikata tiketi ya mashindano hayo yatakayofanyika Rusia mwakani.
Brazil wameishusha Argentina ambao wamekuwa nafasi ya pili baada ya kukalia kiti hicho kwa takriban miezi 12 kwenye viwango hivyo vya Fifa. Hata hivyo mtihani mgumu kwa timu hiyo ni kupambana ili kufuzu kwenye mashindano hayo kutokana na mshambuliaji wake tegemeo Lionel Messi kufungiwa kucheza mechi nne.
MSIMAMO WA FIFA 20 BORA:
1. Brazil
2. Argentina
3. Ujerumani
4. Chile
5. Colombia
6. Ufaransa
7. Ubelgiji
No comments