Header Ads

MAKOCHA 10 WATAKAOWEZA MRITHI WENGER

Kipigo cha  jumla ya mabao 10-2 kutoka kwa Bayern Munich kimezidi kumweka katika hali ngumu kocha wa Arsenal, Arsene wenger.
Kundi la mashabiki na wachambuzi wa soka wanaompinga limezidi kuongezeka na hoja zao kupata nguvu.
Mjadala wa hatma ya Wenger kuendelea kuifundisha Arsenal msimu ujao umekuwa mkubwa kiasi cha wadadisi wa mambo ya soka kuanza kuanika orodha ya makocha wanaoweza kuziba pengo lake ikiwa kocha huyu aliyedumu kwa misimu 21 ataachia ngazi mwishoni mwa msimu huu.
Kocha wa Everton, Ronald Koeman anatajwa kama kinara wa kumrithi Wenger. Koeman, raia wa Uholanzi anapigiwa chapuo kwa kuimarisha Everton tangu iliyoonekana kuyumba chini ya Roberto Martinez.
Muitaliano Massimiliano Allegri wa Juventus naye ameunganishwa katika orodha ya makocha wanaotajwa kumrithi Wenger.
Jina la Jorge Sampaoli, kocha wa sasa wa Sevilla licha ya kutajwa kuwa mstari wa mbele kumrithi Luis Enrique wa Barcelona, limejumuishwa katika orodha ya warithi wa Wenger.
Jina la Diego Simeone wa Atletico Madrid halijasahaulika katika ndimi za wadadisi wa mambo ya soka kuwa mtu sahihi wa kugeuza mwelekeo wa Arsenal endapo klabu hio itaamua kumpa kisogo Wenger.

Wengine ni , Joachim Low wa Ujerumani, Thomas Tuchel wa Borussia Dortmund, Luis Enrique, msaidizi wa Wenger Steve Bould, Eddie Howe wa Bournemouth na Raplh Hasenhuttl wa RB Leipzig
Katia ya hao wewe unaona nani ni bora Zaidi na kustahili kuwa mrithi wa Wenger?

No comments