Header Ads

MESSI AZIDI KUWEKA REKODI ULAYA

Pambano la Ligi ya Mabingwa kati ya Barcelona na Paris Saint-Germain ni kati ya michezo ya kusisimua zaidi katika kwa siku za karibuni.
Penati ya Lionel Messi katika mchezo huo wa marudiano ilimfanya amfikie mpinzani wake wake mkubwa, Crstiano Ronaldo kwa idadi ya mabao 11 ya mikwaju ya penati.
Messi amefikisha mabao 94 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa nyuma ya Ronaldo kwa bao moja. Hata hivyo alikuwa na uwezo wa kumfikia Ronaldo kama asingeamua kumuachia Neymar kupiga penati katika dakika ya 91 kuiandikia Barcelona bao la 5 lililoibua matumaini ya kuiondoa PSG.
Kwa upande wa PSG iliyotolewa kwa jumla ya mabao 6-5 licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza, mshambuliaji wao Edinson Cavani ameifikia rekodi ya Zlatan Ibrahimovic ya kuwafungia wafaransa hao mabao 20 katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments