Wapinzani wa Yanga, timu ya Zanaco kutoka Zambia wameonekana kuweka msisitizo wa wa kupata matokeo mazuri kwa kuizuia Yanga kushambulia Wapinzani wa Yanga, timu ya Zanaco kutoka Zambia wameonekana kuweka msisitizo wa wa kupata matokeo mazuri kwa kuizuia Yanga kushambulia kutokea pembeni.
Zanaco ni timu nzuri jambo ambalo linathibitishwa na kutwaa taji la ligi Zambia na pia wameshawahi kuzitoa timu za Simba na Yanga huku nyuma lakini miaka ya hivi karibuni Yanga imeimarika kiuchumi na kikosi chake kinajumuisha wachezaji wa mataifa mbalimbali ya Afrika. pembeni.
Katika mazungumzo ya benchi la ufundi la Zanaco mara tu baada ya kuwasili nchini, mada kubwa ilijikita katika uimara wa wingi ya kulia ya Yanga.
Mmoja wa viongozi wa Zanaco alikuwa akirudia rudia kuwa mashambulizi mengi ya Yanga yanatokea pembeni hasa upande wa kulia.

Simon Msuva wa Yanga akipiga shuti chini ya ulinzi wa kiungo wa Mtibwa, Henry Joseph katika mojawapo wa mechi za Ligi Kuu
Winga tegemezi, Simon Msuva amekuwa akicheza upande wa kulia mara nyingi akikata ndani kufunga mabao au kuwapikia wenzake.
Kwa mhusika aliyewapokea Zanaco, mabingwa wa Zambia waliowatupa nje APR ya Rwanda wamejipanga kuidhibiti Yanga kwa kuwabana eneo hilo la pembeni kwa njia ya kuweka watu wenye kasi na nguvu pembeni.
” Soka ni mchezo wa vitu vitatu, nguvu, maarifa na kasi. Mambo mengine ni ziada tu ya kuleta burudani. Sisi tunataka matokeo. ” kauli ya mmoja wa wakufunzi wa Zanaco.
Hata hivyo licha ya ukweli kuwa mabao mengi ya Yanga yamekuwa yakitokea upande wa kulia anakocheza Msuva na Juma Abdul, ukweli ni kwamba wawakilishi wa Tanzania hawategemei upande mmoja kwani Obrey Chirwa anacheza zaidi upande wa kushoto na amekuwa akifunga mabao hasa katika siku za hivi karibuni.
Ugumu wa mechi ya Yanga na Zanaco unatokana na ukweli kwamba timu za Zambia zimekuwa zikizinyanyasa timu za Tanzania hasa katika mechi za marudio ambazo mara zote hufanyikia ugenini.

Zanaco ni timu nzuri jambo ambalo linathibitishwa na kutwaa taji la ligi Zambia na pia wameshawahi kuzitoa timu za Simba na Yanga huku nyuma lakini miaka ya hivi karibuni Yanga imeimarika kiuchumi na kikosi chake kinajumuisha wachezaji wa mataifa mbalimbali ya Afrika.

No comments