Katika kile ambacho kinaonekana kama kauli tata, Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa anaweza kupanga kikosi cha wachezaji kadha vijana katika mchezo wa timu yake dhidi ya Arsenal, Jumapili hii.
Manchester United inatarajiwa kuwa ugenini kuivaa Arsenal katika mchezo wa Premier League, Jumapili hii ambapo timu zote zinawania nafasi ya kuingia kwenye nafasi nne za juu ili kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Man United ipo katika nusu fainali pia ya Kombe la Europa na imeshacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Celta Vigo ikashinda bao 1-0, kama ikiingia fainali na kuchukua taji hilo itaingia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya hata kama haitakuwemo katika nafasi nne za juu kwenye Premierm League.
Kwa sasa kikosi cha United kimekuwa kikikabiliwa na majeruhi wengi kiasi cha kumfanya kocha huyo kusema kuwa atawapumzisha mastaa wake kadhaa katika mchezp wa Arsenal ili waelekeze nguvu kwenye mchezo wa marudio dhidi ya Celta Vigo.
Kauli hiyo inaweza kuwa ni tata kwa kuwa kawaida ya Mourinho ni kupenda kuwavuruga wapinzani lakini pia anaweza kufanya hivyo kweli kutokana na uwepo wa wachezaji waliokuwa fiti katika kikosi cha kwanza.

No comments