Msimu wa ligi kubwa barani Ulaya na hata Afrika unaelekea mwishoni, baada ya msimu kuisha kinachofuatia ni usajili ili kujiandaa na msimu ujao wa ligi.
Vilabu nchini Uingereza tayari mapemaa hata ligi haijaisha vimeshaanza kupigana vikumbo kutafuta wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Arsenal na Liverpool nao wamejikuta sasa wakiingia katika vita nzito katika kutafuta saini wa nyota wa Olympique Lyon Alexandre Lacazette ambaye amekuwa akihitajika Arsenal kwa muda sasa.
Baada ya Arsenal kuonekana wanajivuta vuta kumnunua mcheka na nyavu huyo, sasa Liverpool nao wameingia katika vita ya kumtaka Lacazette.
Vita kati ya miamba hao wawili imenogeshwa zaidi baada ya klabu ya Olympique Lyon kuweka wazi kwamba Lacazatte anaweza kuondoka klabuni hapo na kama kuna atakayeweza kupeleka ofa apeleke.
Raisi wa Lyon Jean Michel amenukuliwa akisema “kuna mchezaji mmoja tu mwenye ruhusa ya kuondoka Lyon naye ni Alexandre Lacazette lakini hiyo haimaanishi kwamba anaondoka”
Michel anasema klabu yoyote inayomtaka ni lazima waelewane nao ndio aondoke, lakini Liverpool na Arsenal wanaweza kukabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa miamba ya Hispania klabu ya Atletico Madrid.
No comments