Header Ads

GERARD PIQUE AKOSA MAZOEZI YA WIKI NZIMA, KISA HAKIJULIKANI

Licha ya kupewa siku mbili za kupumzika lakini beki wa kati wa Barcelona, Gerard Pique ameshindwa kufanya mazoezi na kikosi cha timu yake kwa wiki nzima.
Kutokana na hali hiyo kuna uwezekano mkubwa wa Pique kuukosa mchezo dhidi ya Las Palmas, kesho Jumapili katika La Liga.

Imefahamika kuwa Kocha wa Barcelona, Luis Enrique tayari ameshawaita wachezaji kutoka kikosi cha vijana Marlon Santos, Carles Alena na Wilfried Kaptoum, ili kuziba nafasi ya mkongwe huyo.

Bado hakuna tamko rasmi ya kipi kilichosababisha mchezaji huyo kukosekana mazoezini kwa muda wote huo.

No comments