Header Ads

JOHN BOCCO ATHIBITISHA KUONDOKA AZAM FC, AONYESHA CHOZI

Kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar inaonekana bado kinaitesa Azam FC, ambapo zile taarifa za nahodha wa timu hiyo, John Bocco kutimuliwa sasa zipo 'live'.
Taarifa hizi zilianza kusambaa jana mara baada ya mchezo huo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom, ambapo ilielezwa pia hata kocha mkuu wa timu hiyo naye ameonyeshwa mlango wa kutokea.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bocco ambaye ni mchezaji mkongwe kikosini hapo amekiri hilo katika staili tofauti.
Bocco ameweka video fupi ya Kihindi ya mwanadada akipanda treni akimwaga machozi huku akibembelezwa kubaki na mwanaume lakini anakataa.
Kisha chini ya video hiyo kuliambatana na maneno yanayosema:
"Kuna wakati wa kuondoka, ondoka wajue thamani yako hata kama huna pa kwenda.
Kocha wa Azam FC, Cioba Arastica alisaini mkataba wa muda mfupi klabuni hapo hivi karibuni.
Azam FC imemaliza msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom 2016/17 kwa kushika nafasi ya nne katika ligi hiyo nyuma ya Yanga, Simba na Kagera Sugar.

No comments