Juventus imeitoa nishai Monaco baada ya usiku huu kuifunga mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya uliochezwa kwenye dimba la Stade Louis II huko jijini Monaco nchini Ufaransa.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Lahoz kutoka Hispania ilishuhudiwa Juventus ambao walikuwa wageni kwenye mchezo wa leo wakipata mabao yao katika kipindi cha kwanza na cha pili kupitia kwa mshambuliaji wao wa kimataifa kutoka nchini Argentina,Gonzalo Higuaini aliyefunga katika dakika za 29 na yote yakitokana na krosi safi za mlinzi wa kulia wa kimataifa kutoka Brazil,Dani Alves aliyekuwa akipanda mara kwa mara kusaidia mashambulizi.
Ushindi huo muhimu umeiweka Juventus katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo kwani katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumanne ijayo huko jijini Turin nchini Italia,miamba hiyo itahitaji matokeo ya ushindi wowote ama sare ili iweze kukata tiketi ya kuelekea jijini Cardiff,Wales ambako bingwa wa michuano hiyo atatafutwa.
No comments