Goli lililoweka rekodi ya kufungwa mapema zaidi kwenye Ligi Kuu Tanzania bara mpaka sasa, lilifungwa Ijumaa iliyopita kwenye mechi ya Ligi Kuu kati ya Simba dhidi ya Stand United.
Lilifungwa sekunde ya 16 na kiungo Selemani Kassim Selembe wa Stand kwenye mechi iliyoisha kwa Simba kushinda mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwenye soka lolote linaweza kutokea, lakini kwa jinsi mechi za Ligi Kuu zilivyobaki chache, huenda likabaki kuwa ndiyo goli lililofungwa mapema zaidi msimu huu wa 2016/17.
Yafuatayo ni magoli 10 yaliyofungwa mapema zaidi msimu huu na majina ya wachezaji waliofunga.

1. Lambart Subianka-Prisons (dakika ya 8)
Straika huyu wa Prisons ndiye mchezaji aliyeweka rekodi ya kufunga bao la kwanza msimu huu. Alifanya hivyo dakika ya nane ya mchezo kwenye mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Agosti 20 mwaka jana likiwa ni bao pekee dhidi ya Majimaji, Prisons ikiwa ugenini.
2. Abdulrahman Mussa-Ruvu Shooting (dakika ya 8)
Ni straika tegemeo wa Ruvu Shooting. Naye aliweka rekodi ya kufunga bao la mapema Septemba 7 mwaka jana, mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Simba, Uwanja wa Uhuru.
Alifunga dakika ya nane ya mchezo, lakini timu yake ikilala mabao 2-1 dakika 90 zilipomalizika.
Alifunga dakika ya nane ya mchezo, lakini timu yake ikilala mabao 2-1 dakika 90 zilipomalizika.
3. Haruna Shamte-Mbeya City (dakika ya 7)
Beki wa Mbeya City, Haruna Shamte alifunga goli dakika ya saba ya mchezo Agosti 28 kwenye mechi kati ya timu yake dhidi ya Toto African, Uwanja wa CCM Kirumba, Mbeya City ikishinda bao 1-
4. Haruna Chanongo-Mtibwa Sugar (dakika ya 6)
Winga wa Mtibwa Sugar, Haruna Chanongo anaingia kwenye rekodi ya kufunga bao la mapema, alipofunga goli dakika ya sita ya mchezo kati ya timu yake dhidi ya Kagera Sugar. Mechi hiyo ilichezwa Septemba 17 mwaka jana, Mtibwa ikishinda mabao 2-0.
5. Amissi Tambwe-Yanga (dakika ya 5)
Septemba 17 mwaka jana, straika wa Yanga, Amissi Tambwe alifunga bao dakika ya tano, Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Yanga ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Mwadui FC.
6. Ibrahim Jeba-Mtibwa (dakika ya 2)
Kiungo Ibrahim Jeba wa Mtibwa alifunga bao dakika ya pili ya mchezo kwenye mechi iliyochezwa Uwanja wa Manungu, Turiani, dhidi ya Kagera Sugar, Septemba 17 mwaka jana. Mtibwa ilishinda mabao 2-0, la kwanza likifungwa na Chanongo dakika ya sita.
7. John Bocco-Azam FC (dakika ya 2)
Straika wa kutegemewa wa Azam FC, John Bocco alipachika bao dakika ya pili ya mchezo kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Majimaji Uwanja wa Azam Complex. Ilikuwa ni Agosti 27 mwaka jana, Azam ikishinda mabao 3-0.
8. Yusuph Ndikumana-Mbao (sekunde ya 46)
Mchezaji huyu anayecheza nafasi ya ulinzi wa kati, wakati mwingine kiungo wa kukaba, aliweka rekodi ya kufunga bao la mapema sekunde ya 46, Uwanja wa CCM Kirumba, Februari 2 mwaka huu, timu yake ikicheza dhidi ya Mtibwa Sugar.
Aliisaidia timu yake ya Mbao FC kushinda mabao 5-0 kwenye mechi hiyo.
Aliisaidia timu yake ya Mbao FC kushinda mabao 5-0 kwenye mechi hiyo.
9. Selemani Selembe-Stand United (sekunde ya 16)
Akitumia makosa ya mabeki wa Simba na kipa wao Daniel Agyei, Selembe alifunga bao la mapema zaidi, sekunde ya 16, linaloongoza kuwa la mapema zaidi kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka saa, mechi ikichezwa Mei 12, Simba ikishinda mabao 2-1.

No comments