Header Ads

MALI 0-0 SERENGETI BOYS ‘LIVE’ FULL TIME, KUTOKA GABON

Mwamuzi anamaliza mchezo, matokeo ni 0-0.
Dakika ya 92: Mali wanapata kona, inapigwa lakini kipa wa Serengeti anafanya kazi nzuri anaudaka.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika mbili za nyongeza.
Dakika ya 90: Mali wanafanya shambulizi lakini mpira unakuwa na kasi kubwa unatoka nje, inakuwa goal kick.
Dakika ya 85: Mchezo unaendelea, mpira unachezwa katikati ya uwanja muda mwingi.
Dakika ya 82: Mchezo umesimama kwa muda, kuna mchezaji wa Serengeti yupo chini akipatiwa matibabu.
Dakika ya 80: Mchezo unaendelea lakini Mali ndiyo ambao wanafanya mashambuliz mara kadhaa.
Dakika ya 72: Beki wa Serengeti Dickson anaumia mwenyewe mguu, anatolewa nje kupatiwa matibabu. Baada ya muda anarejea.
Dakika ya 72: Abdul Seleiman ameshindwa kurejea uwanjani, nafasi yake unachukuliwa na mchezaji mwingine.
Dakika ya 70: Abdul Seleiman anaumia kichwani wakati wa kuwania mpira, anatolewa nje kupatiwa matibabu.
Dakika ya 67: Mchezo unaendelea kwa kasi, Serengeti wanajaribu kujipanga lakini pasi zao kadhaa hazifiki kwa walengwa.
Dakika ya 65: Mali wamelisakama lango la Serengeti, wanarejea na nguvu na kushambulia lakini walinzi wa Serengeti wanakuwa makini.
Dakika ya 63: Mshambuliaji wa mali anawapiga chenga walinzi wa Serengeti na kupiga mpira unakuwa kona.
Dakika ya 60: Mali wanafanya shambuli lakini mpira unatoka nje.
Dakika ya 53: Serengeti wanafanya shambulizi lakini shuti linakuwa na nguvu ndogo kipa anadaka.
Dakika ya 50: Serengeti Boys wanaanza kufunguka na kucheza pasi nyingi, wanasogea kwenye lango la Mali.
Dakika ya 48: Mchezo umeanza kwa timu zote kusomana.
Kipindi cha pili kimeanza.
Serengeti Boys wanafanya mabadiliko, anaignia Abdul Suleiman, anatoka Mohamed Abdallah
Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili.
MAPUMZIKO
Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza.
Dakika ya 46: Serengeti wanapata faulo nje ya eneo la 18 la Mali, linaopigwa shuti lakini linapaa juu ya lango.
Dakika 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika moja ya nyongeza.
Dakika ya 41: Beki wa Serengeti, Ally Msengi anafanya makosa na kusababisha Serengeti kushambuliwa lakini shuti linatoka nje ya lango.
Dakika ya 39: Serengeti wanaanza kujipanga vizuri wanafanya shambulizi lakini kipa wa Mali anauwahi mpira.
Dakika ya 35: Serengeti wanahitaji kuwa makini zaidi, muda mwingi mpira unachezwa kwenye lango lao.
Dakika ya 32: Mabeki wa Serengeti wanafanya uzembe, wanamrudishia kipa mpira lakini straika wa Mali anauwahi na kutaka kufunga, kipa anafanya kazi kubwa kuokoa, mpira unamkuta straika mwingine anatupia mpira wavuni lakini tayari anakuwa ameshaotea.
Dakika ya 29: Mali wanapata kona, inapigwa kona juu straika wa Mali anamchezea faulo kipa wa Serengeti, Ramadhani Kabwili na mwamuzi anapuliza kipenga, inakuwa faulo kuelekea kwa Mali.
Dakika 23: Mali wanafanya shambulizi lingine la nguvu lakini walinzi wa Serengeti wanakuwa makini kuondoa hatari.
Dakika ya 20: Mchezo bado hauna kasi kubwa lakini ni vijana wa Mali ndiyo ambao wamemiliki mpira muda mwingi.
Dakika ya 16: Mali wanafanya shambulizi kali langoni mwa Serengeti lakini mpira unatoka nje.
Dakika ya 10: Mali wamefila langoni mwa Serengeti Boys mara mbili.
Dakika ya 5: Timu zote zimeanza mchezo kwa kasi ndogo zikisomana.
Dakika ya 1: Mchezo ndiyo kwanza umeanza.
Mchezo unachezwa kwenye Uwanja wa Stade de l'Amitié Sino-Gabonaise jijini Libreville, mwamuzi wa kati ni Ferdinand Udoh Aniete wa Nigeria.
Timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 ipo uwanjani kucheza dhidi ya wenzao wa Mali katika mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika ya Vijana U17. Mchezo huu ni wa Kundi B. Unatarajiwa kuanza muda si mrefu  kutoka sasa.

No comments