Header Ads

MAN U YAZIDI KUDAIWA

Deni la klabu ya Manchester United limezidi kuongezeka kutokana kuimarika kwa dola ya Marekani dhidi ya pauni ya Uingereza katika soko la ubadilishaji fedha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Manchester United, deni la klabu hio limekuwa kwa pauni milioni 17.6 na kufikia pauni milioni 366.3
Mapato ya kibiashara yameongezeak kwa pauni 700,000 na kufikia pauni milioni 66.5 huku pato la udhamini nalo likiongezeka kwa asilimia 2.1

No comments