Header Ads

Manchester United yafanya usajili wao wa kwanza.

Klabu ya Manchester United imekuwa ikipambana kila kukicha kujaribu kurudisha heshima yao ambayo imeshuka kwa muda mrefu tangu Sir Alex Ferguson astaafu.
United wamekuwa wakitafuta wachezaji wengi wenye majina makubwa ili kukiboresha kikosi chao, Griezman,Rodriguez na Moratta ni kati ya wanaotajwa kujiunga na United.
Lakini wakati watu wakifikiria dirisha la usajili kuanza, tayari Manchester United wameshapiga hatua moja mbele kwa kufanya usajili wa kwanza hata kabla dirisha la usajili halijaanza.
United wamemsajili Arnau Puigmal kutoka Espanyol, Puigmal mwenye miaka 16 ni kati ya makinda ambao wamekuwa wakizungumiwa sana kuwa kati ya vipaji vitakavyokuja kusumbua siku za baadae.
Ripoti zinasema Arnau Puigmal alisafiri hadi Uingereza kufanya mazungumzo ya mwisho na United ambapo tayari kila kitu kimekamilika kilichobaki ni kutangazwa tu kwa jambo hilo.
Manchester United wamewapiku wapinzani wao wakubwa na majirani zao kutoka jiji la Manchester timu ya Manchester City ambao walikuwa wakimuwinda Puigmal.

No comments