Kijana mwenye umri wa miaka 18, Kylian Mbappe ambaye amekuwa akiwaniwa na vigogo kadhaa wa Ulaya, habari ni kuwa ameshakubali kwenda Real Madrid.
Chipukizi huyo raia wa Ufaransa, amekuwa akiwaniwa na Manchester United, Arsenal, Real Madrid na Manchester City kutokana na kuonyesha kiwango kizuri kikosi chake cha Monaco.
Gazeti la Marca la Hispania limetaarifu kuwa mchezaji huyo amekataa kwenda England na nia yake ni kucheza katika kikosi cha Madrid ambapo kuna Kocha Zinedine Zidane ambaye ni Mfarans mwenzake.
Pamoja na taarifa hizo hakuna tamo rsmi kutoka kwa Monaco au Madrid lakini tayari Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ameshaweka wazi nia yake ya kumsajili Mbappe ambaye ameshafunga mabao 22 katika mechi 36 za msimu huu.
Inaelezwa usajili huo unaweza kuwa na thamani ya pauni milioni 85.
No comments