Kikosi cha Mbeya City FC, kilitarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam, jana jioni tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji wao Young Africans ‘Yanga’ uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Uhuru, keshokutwa Jumamosi hii.
Ikiwa Yanga haitapata ushindi katika mchezo huo basi mipango yao ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo unaweza kuingia doa kutokana na kuwa kwenye mbio za ubingwa dhidi ya Simba.
Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten ameifahamisha mbeyacityfc.com kuwa jumla ya nyota 18 na viongozi 10 walitarajiwa kuwepo kwenye msafara huo kwa ajili ya kuhakikisha Mbeya City inafanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu na kujiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi.
Ligi iko kwenye hatua za mwisho, huu ni mchezo muhimu, tunataka kushinda na kupata matokeo muhimu kwenye mchezo wa Jumamosi, tunafahamu Yanga ni timu nzuri na iko kwenye mbio za ubingwa lakini hilo halitupi hofu kwa sababu sisi pia tuna kikosi kizuri, tulipata matokeo duru ya kwanza na sasa tunakwenda Dar kuhitimisha dhamaira yetu ya kupata poiti sita msimu huu kutika kwao
Akiendelea zaidi Ten alisema Mbeya City imekuwa na wiki nne za kujiandaa vizuri kuivaa Yanga kwa kufanya mazoezi mazito ikiwa ni pamoja na kucheza michezo zaidi ya mitano ya kirafiki ambayo imesaidia kuimarisha uwezo wa nyota wa kikosi kiuchezaji na kuwaongezea morari ya kutaka kushinda kwenye Uwanja wa Uhuru.
“Tumekuwa na wiki nne za kujindaa, hatukucheza mchezo wowote baada ya sare ya 1-1 na African Lyon kwenye Uwanja wa Sokoine, Aprili 13, hivyo nguvu zetu zote tunaziweka siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru,” alisema Ten.
No comments