Header Ads

MKONGWE ZLATAN IBRAHIMOVIC AFUNIKA KWA UTAJIRI UINGEREZA ANASHIKA NAFASI YA PILI

Dereva wa magari, Lewis Hamilton bado ni mwanamichezo tajiri zaidi nchini Uingereza lakini kwa ukaribu anafuatiwa na straika wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic katika wanamichezo 10 wenye uwezo wa kifedha.
Dereza huyo wa mashindano ya magari anayeendesha magari ya Mercedes kamika michezo ya Formula One ana utajiri wa pauni milioni 131 huku ikionekana ameongeza utajiri wa pauni milioni 25 katika miezi 12 iliyopita.
Ibrahimovic, ambaye ana umri wa miaka 35, amemuacha staa mwingine wa timu yake, Wayne Rooney katika orodha hiyo ambapo imeelezwa kuwa Zlatan ana utajiri wa pauni milioni 110 akiwa na rekodi ya kucheza katika klabu nyingi kubwa za Ulaya zikiwemo Paris Saint-Germain, AC Milan, Barcelona, Juventus na Inter Milan.
Wengine walioingia katika tano bora ni madereva wa Formula One,  Jenson Button na mchezaji wa golf, Rory McIlroy wenye utajiri wa pauni milioni 86 na pauni milioni 82.
Rooney ana utajiri wa pauni 93m wakati Kocha wa Manchester United,  Jose Mourinho anashika nafasi ya saba akiwa na utajiri wa pauni 61, Kocha wa Manchester City,  Pep Guardiola anashika nafasi ya tisa kwa pauni 50m.

No comments