Header Ads

MOURINHO KWELI KAPINDA, APOTEZEA MAZOEZI YA MAN U, AAMUA KULALA KWENYE BENCHI

Inajulikana wazi kuwa Kocha Jose Mourinho hana mpango wa matokeo yatakayotokea kwa timu yake ya Manchester United itakaposhuka uwanjani kucheza mechi yake ya mwisho ya msimu huu katika Premier League dhidi ya Crystal Palace, lakini sasa amefika mbali.
Timu hizo zinakutana Jumapili hii kwenye Uwanja wa Old Trafford, ambapo katika kuonyesha hana mpango na mchezo huo kwanza alishasema atawapanga wachezaji chipukizi katika mchezo huo na wakubwa wachache.

Lakini katika mazoezi ya Ijumaa hii, Mourinho alionyesha utani mwingine kwa kuamua kulala kwenye benchi badala ya kusimamia.

Inajulikana wazi kuwa kocha huyo raia wa Ureno anaiwaza fainali ya Europa League dhidi ya Ajax itakayochezwa Jumatano ijayo.

No comments