Header Ads

MSUVA YAMKUTA MWANZA, MASHABIKI WAMVAA WAKATI WA SHEREHE ZA UBINGWA

Yanga imefanikiwa kukabidhiwa kombe la Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Jumamosi hii, lakini kilichotokea  baaada ya mchezo huo ni balaa.
Mara baada ya mchezo huo, wachezaji wa Yanga walikabidhiwa fulana maalum za ubingwa kwa kuwa ilikuwa imeshajulikana tangu mapema kuwa watakabidhiwa kombe la ubingwa, walipokabidhiwa, ndipo furaha ikazidi kipimo na kusababisha mashabiki wa Yanga kuvamia uwanjani hapo.
Mashabiki hao waliokuwa wamevaa nguo za njano, wengi wao walikuwa na furaha na kuwafuata wachezaji wao kadhaa kwa ajili ya kushangilia pamoja na kupiga picha, lakini ghafla wakamuona Simon Msuva, ndipo wakamvaa na kumbeba.
Msuva ambaye bado alikuwa na bandeji juu ya jicho iliyotokana na kuchanika katika mchezo wa wiki jana, alikuwa akitabasamu tu huku mashabiki hao wakimbeba juu kwa juu na kumrusha huku wakimzungusha uwanjani hapo kiasi cha kuhatarisha usalama wake na mali zake.
Ilibidi mchezaji huyo ambaye pia ameibuka kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa 2016/17 apate msaada wa askari kushushwa chini na  baadaye kujumuika nawenzake.

1 comment: