Header Ads

TETESI ZA USAJILI ULAYA HIZI HAPA

Bellerin: Albert Botines ambaye ni wakala wa mlinzi wa kulia wa Arsenal,Hector Bellerin amekiri kuwa amepokea ofa kwa ajili ya mteja wake huyo lakini si kutoka katika klabu yake ya zamani ya Barcelona kama ilivyoripotiwa hapo kabla. Bellerin,23,amekuwa akihusishwa na mpango wa kutaka kuondoka Arsenal katika siku za hivi karibu hasa baada ya Kocha Arsene Wenger kushindwa kuweka wazi hatima yake kama ataondoka ama atabaki klabuni hapo.


De Roon:Everton imeelezea nia yake ya kutaka kumsajili kiungo wa Middlesbrough, Mholanzi Marten de Roon limeandika gazeti la Daily Mail.De Roon,26,ameonyesha kiwango bora tangu alipojiunga na Middlesbrough msimu uliopita akitokea Atalanta ya Italia.Dau la £12m limedauwa kuwa litaishawishi Middlesbrough kumwachia kiungo huyo wa nguvu.


Kocha wa Everton,Mdachi Ronald Koeman amepewa ruhusa na klabu hiyo kuanza mipango ya kumsajili straika wa Malaga,Sandro pamoja na kiungo wa Ajax,Davy Klaassen.Limeandika The Mirror.Sandro ambaye ni nyota wa zamani wa Barcelona amedaiwa kuwa na thamani ya £5 huku dau £20m likidaiwa kuwa litaishawishi Ajax kumwachia Klaassen ambaye ni nahodha wake.


Coutinho:Kocha wa Liverpool,Jurgen Klopp amesisitiza kuwa kiungo wake mahiri Philippe Coutinho atabakia klabuni hapo licha ya kutakiwa kwa udi na uvumba na klabu ya Barcelona ya nchini Hispania.Mwezi Januari Coutinho,24,alisaini mkataba wa miaka mitano wa kusalia Anfield lakini hilo bado halijaikatisha tamaa Barcelona.



Hart:Kipa wa Manchester City anayecheza kwa mkopo Torino ya Italia,Joe Hart huenda kwa mara nyingine akabiliwa na changamoto ya kupata timu mpya msimu ujao baada ya matakwa yake ya mshahara pamoja na ada lake la uhamisho kuzitisha timu nyingi barani Ulaya.Manchester City inataka dau la £30m huku Hart mwenyewe akitaka alipwe mshahara wa £120,000 kwa wiki.(Manchester Evening News)



Stam:Kocha wa Reading,Mdachi Jaap Stam amesema hajui kama atakuwa klabuni hapo msimu ujao.Stam ametoa kauli hiyo baada ya hivi karibu kuanza kunyatiwa na vilabu vya ligi kuu England kutokana na kuiwezesha Reading kushika nafasi ya tatu Championship.

No comments