Wakati sakata lake la usajili likiendelea kuwa gumzo, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amefichua siri kuwa kumbe aliwahi kumfuata Kylian Mbappe hadi nyumbani kwao ili amshawishi ajiunge na Arsenal.
Wenger amesema kuwa klabu yake ilikuwa ikimfuatilia mchezaji huyo kwa muda kabla ya kuweka wazi nia yao hiyo.
Mbappe ambaye anaichezea Monaco amekuwa na msimu mzuri katika timu yake ya Monaco kiasi cha kuwa kivutio kwa timu kubwa nyingi za Ulaya.
"Hata yeye mwenyewe anaweza kuwaambia kuwa nilifika kwao mwaka jana kwa kuwa alikuwa anaelekea kumaliza muda wa mkataba wake, lakini Monaco wakamshawishi kuongeza mwingine na ikawa ngumu kumpata.
"Nilielewa kwa kuwa alikulia pale na mwisho akaamua kuendelea kubaki Monaco," alisema Wenger.
No comments