Header Ads

YANGA YAFUNGUKA KUHUSU TUZO

Klabu ya Yanga SC imewapongeza wachezaji wake Saimoni Msuva na Haruna Niyonzima kwa kuondoka na tuzo katika hafla ya ugawaji tuzo za Ligi kuu Tanzania Bara katika msimu uliomalizika wa 2016/17.

Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Idara ya habari na mawasiliano ya klabu hiyo kwa kusema wanajivunia wachezaji hao kupata tuzo hizo kwani mafanikio ni chachu katika kuendelea kufanya vizuri katika mashindano yao kiujumla.

"Uongozi wa klabu ya Yanga SC pamoja na benchi la ufundi unatoa pongezi za dhati kwa wachezaji wetu Saimoni Msuva aliyeibuka mfungaji bora wa ligi kuu pamoja na Haruna Niyonzima aliyenyakua tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ....Mafanikio yenu ndio chachu ya mafanikio ya klabu yetu....Tunajivunia hilo sambamba na wenzenu wote kwenye kikosi kwa kujituma kwa moyo wote kuhakikisha timu yenu inakuwa mabingwa wa ligi kuu mara tatu mfululizo". Ilisema taarifa hiyo

Niyonzima ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda Method Mwanjale kutoka Simba na Yusuph Ndikumana wa Mbao FC huku Saimon Msuva akiwa sawa na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting baada ya kuwa na idadi sawa ya magoli msimu huo.

No comments