Header Ads

REAL MADRID YAKUBALI KUMUUZA RONALDO KWA MKWANJA USIOPIMIKA


Image result for ronaldo

Real Madrid wamesema timu itakayomtaka Ronado italazimika kulipa pauni milioni 350.
Real wana matumaini kuwa bei hiyo huenda ikawakatisha tamaa Paris Saint Germain na Manchester United zinazomtaka Ronaldo lakini washauri wa Ronaldo wanasema ada ya pauni milioni 131 itatosha kumsajili mchezaji huyo ambaye anataka changamoto mpya.

Chelsea wameibuka na kusema wanamtaka Cristiano Ronaldo, huku mmiliki Roman Abramovic akisema yuko tayari kuvunja rekodi ya dunia ya usajili.

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amemuambia Ronaldo kuwa hatomzuia iwapo anataka kuondoka Spain.

Ronaldo atabakia Real Madrid iwapo klabu hiyo itakubali kumlipia kodi anayotuhumiwa kudaiwa ya pauni milioni 13.

Paris St-Germain wanajiandaa kumfanya Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji aghali zaidi duniani, baada ya kusikia kuwa anataka kuondoka Madrid.

Manchester City nao wamewasiliana na Cristiano Ronaldo baada ya kusikia kuwa anataka kuondoka Real Madrid.

No comments