Header Ads

UEFA YATANGAZA KUTOA TUZO TANO MWEZI AGOSTI

Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) limetangaza kuanza kutolewa kwa tuzo tano mpya za wachezaji bora wa mwaka kuanzia Agosti hii ambazo washindi wake watapatikana kutokana na kura za makocha na wanahabari.
Tuzo hizo zitakabidhiwa jijini Monaco nchini Ufaransa hapo Agosti 24 wakati wa droo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tuzo hizo 5 mpya ni kwa wachezaji waliofanya vyema kwenye mashindano ya klabu ya UEFA kwa msimu uliopita, kwa mwaka 2016/17,na zitatolewa sambamba na za mchezaji bora wa mwaka kwa wanaume na na wanawake.

No comments