Header Ads

TANZANIA YAPOROMOKA NAFASI TANO FIFA

TANZANIA imeshuka nafasi tano katika viwango vya soka duniani vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), huku Ujerumani ikichumpa hadi nafasi ya kwanza.
Julai mwaka huu, Tanzania ilipanda hadi nafasi ya 114 kabla ya kuporomoka hadi nafasi ya 120 Agosti mwaka huu na kushuka zaidi mwezi huu huku Uganda ikipanda kwa nafasi mbili kutoka 73 hadi 71 wakati Kenya ikishuka  kutoka nafasi ya 82 hadi ya 88 katika viwango hivyo.
Orodha hiyo iliyotolewa jana na FIFA, ilionyesha kuwa Uganda inaongoza ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikifuatiwa na Kenya iliyopo nafasi ya 88, Rwanda 118, Tanzania 125, Burundi 129, Sudan 134, Ethiopia 144 na Sudan Kusini 150.
Pia orodha hiyo ilionyesha nchi ya Misri inaongoza Afrika kwa kuwa nafasi ya 30, ikifuatiwa na Tunisia nafasi ya 31 wakati Senegal inashika nafasi 33, Congo DRC ya 42, Nigeria 44, Cameroon 45, Burkina Faso 49, Ghana 52, Ivory Coast 54 na Morocco iliyoko nafasi ya 56.
FIFA iliitaja Ujerumani kuwa kinara wa viwango vya soka duniani ikifuatiwa na Ujerumani, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Poland, Switzerland, Ufaransa, Chile na Colombia huku nchi ya Tonga, Somalia, Gibraltar na Eritrea zikiwa za mwisho kwenye orodha hiyo.

No comments